Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 27 YA 31

Je, umetambua kwamba kuamua kusoma Biblia kila siku ni moja ya maamuzi ya kimkakati ya kupata furaha? Biblia ina nguvu isiyoisha kuliko majibu yoyote ya kibinadamu kwa magonjwa.

Biblia si kitabu cha kawaida. Ni chanzo cha nguvu ya mbinguni. Watu wengi huniambia kwamba hawaielewi Biblia...na nawaambia ni kweli! Wewe endelea kusoma tuu! Hatusomi siku zote neno la Mungu kwa ajili ya kupata taarifa ila tunasoma siku zote kwa ajili ya kupata mabadiliko! Nakuhakikishia kile ambacho akili yako kuelewa, roho yako inaelewa.
Kwa sababu huna adui...na anaelewa nguvu mkristo anayoipata kwa kusoma Biblia...shetani atafanya kila analoweza kukushawishi usisome neno la Mungu.

Nidhamu siyo kitu chepesi, siku zote inahitaji dhamira ya kweli. Usitafute visingizio vya kwa nini hukusoma Biblia jana au leo huwezi kusoma leo...wewe soma! Fanya maamuzi ya kutumia muda wako kila siku kwenye neno la Mungu, na utakuwa na furaha sana kushirikiana na ulimwengu unaokuzunguka!

Maombi yangu kwako leo ni utatangaza na Nabii Yeremia, "Maneno yako yalifanyika furaha na kicheko moyoni mwangu!"
siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com