Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 100

100
Nchi zote Zaitwa Kumsifu Mungu
Zaburi ya Shukrani.
1Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
2Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba;
3 # Ayu 10:8,9; Mhu 12:1; Efe 2:10; Eze 34:30 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 # 1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 106:1; 107:1; 118:1; 136:1; Yer 33:11 Kwa kuwa BWANA ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 100: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia