Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 24 YA 31

Siku moja, nikiwa chuoni, nilipata mwaliko wa kutisha kutoka kwa Mkuu wa Chuo wa chuo cha kikristo nilichokuwa nasoma. Niliomba kubadilisha masomo yangu kwa kuchelewa, na huyo mkuu alitaka kujua kama najua madhara ya kufanya hivyo kwamba naweza nisifuzu masoma yangu kwa wakati. Katibu wake alinipigia simu bwenini na kuniarifu siku na wakati naotakiwa kufika.

Nilipokuwa natembea kuelekea ghorofa ya sita katika jengo la utawala, mdomo wangu ulikuwa umekauka, tumbo linaniuma, na magoti yangu yalikuwa yanagongana. Nilikuwa nawaza nini?! Niliwezaje kufikiria uamuzi wa kijinga kiasi hicho mpaka Mkuu wa Chuo aniite kwenye ofisi yake binafsi?!

Nilipofika eneo la jengo ambapo ofisi ya huyu Mkuu alikuwa anafanya kazi, katibu wake aliniongoza kwenye ofisi ya kifahari ya huyu Mkuu. Aliniarifu kwamba atarejea punde tuu kwa hiyo naweza kukaa.

Nilipokuwa naangaza macho ofisini kwake siku ile, niliona vyeti mbalimbali kutoka kwenye vyuo maarufu sana kwa wakati ule. Alikuwa amepata shahada nyingi sana katika maisha yake kuliko vyeti vyote vya familia yangu, pamoja na mashangazi, wajomba, na mabinamu ambavyo hawajawaza hata kuwa navyo.

Lakini picha iliyonivutia sana haikuwa stashahada au cheti. Ilikuwa ni picha ya Mkuu wa Chuo alishikana mkono na watu maarufu au wasomi maarufu. Picha iliyonipa msisimko ndani ya moyo wangu ilikuwa ni picha ya Yesu... kichwa chake kikiwa kimeguka nyuma kwa kicheko na tabasamu lake. Chini ya picha hii kulikuwa na maandishi " Mungu wako anakufurahia!"

Je, unatambua kwamba furaha ni moja ya sifa za Mungu mwenyewe? Furaha ni kiungo cha tabia ya Mungu. Kuna furaha kubwa kwa kila anachofanya na hamasa kubwa kwa kila anachoahidi kufanya.

Ni nini hasa kinachomfanya Mungu ajawe na furaha? Jibu lake litakunyeyekesha... wewe ndiye kitu kinachomjawa muumba wa mbingu na nchi furaha! Mungu anakufurahia kama bwana harusi anavyomfurahia bibi harusi wake.

Mungu anafurahinsana kuwa na uhusiano na wewe na hujikuta anaimba juu yako!
siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com