Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 23 YA 31

Paulo, mwanatheologia mkuu na mwinjilisti ambaye bado hajatokea kama yeye, yuko tena katika matatizo. Amekamatwa akihubiri neno la Mungu mahali pasipo sahihi na wakati usio sahihi. Hata hivyo, kabla ya kumtupa gerezani, mfalme Agripa mwenyewe aliamua kusikiliza upande wa Paulo. Agripa aliletwa ukumbini katika fahari yake yote na kuketi kati ya viongozi wa kisiasa wa wakati ule.

Kadri umati ulivyokuwa unanyamaza mbele ya mfalme wa duniani, mfalme Agripa aliyejulikana kama mfalme mwenye nguvu na mwenye amri, aligeuka na kumwangalia Paulo na kumtaka ajitete.

Ungekuwa wewe ungefanyaje katika mazingira haya? Ki ukweli, moyo wangu ungekuwa unadunda kwa nguvu sana! Wengi wetu wangekuwa wanajiuliza Mungu sasa yuko wapi katikanhali hii! Kweli Mungu?! Nimekuwa nahubiri injili kwa jna lako na sasa natakiwa kujitetea mwenyewe mbele ya huyu mtu mwenye nguvu?!

Najua ningekuwa namwomba Mungu nisitapike au kuzimia mbele ya mtu huyu ambaye anaweza akaamuru niuwawe au nihukumiwe kwenda kwenye gereza la Kirumi kwa kutikisa kichwa chake tuu. I

Paulo kwa utulive alinyoosha mkono wake kuelekea upande wa Agripa na kuanza moja ya utetezi wake fasaha kwa maneno haya "ninafurahi mfalme Agripa, kwa sababu nitajitetea mwenyewe leo mbele yako na kugusia mambo yote ninayoshitakiwa kwayo na Wayahudi" Matendo ya Mitume 26:2

Paulo kwa ujasiri anasemammbele ya mtu huyu mwenye nguvu sana nyakati hizo kwamba " najiona mwenye furaha..." utakapokuwa katika magumu, utajiona mwenye furaha?

Utakapokuwa katika hali ngumu, unaonaje ukijiona mwenye furaha?

Wakati maisha yako yanakaribia kupasuka, kwa nini usijaribu, kama Paulo alivyofanya, kujiona mwenye furaha?

Tunaweza kubadili jinsi tunavyofikiri kwa sababu tunamjua Yesu Kristo. Tunaweza kubadili jinsi akili zetu zinavyotazama mazingira kwa sababu tunajua kwamba Mungu muumba siku zote atatupa neno la mwisho! Nakuamini...jione mwenye furaha leo!
siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com