Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 22 YA 31

Je, uko tayari kwa mafunzo ushauri katika kumbukumbu ya historia? Je, uko tayari kwa mpango utakaokufanya uwe na uwezo wa kutembea katika ushindi na kutokuwa tena mhanga wammsongo wa mawazo au kukata tamaa? Kama ndiyo... basi kujitoa wako ni leo!

"Endelea kufurahi!" Ni agizo la Agano Jipya linalomaanisha haina uchaguzi! Mpango mkakati wako wa ushindi in kuendelea kufurahi!"

Furaha siyo tu kitendo cha utii kwa Mungu. Furaha ni utii kwa Mungu!

Furaha ni kitendo cha utii na tumeamriwa kufurahi katika Bwana na Kufurahia katika uwepo wake.

C. S. Lewisi alisema namna hii, Ni wajibu wa mkristo kila mmojamkuwa na Furaha kwa kadri anavyoweza.

Lengo kuu la maisha yako ni kumtukuza Mungu kila siku unayoishi. Lengo la maisha yako ni kuliheshimu jina lake kwa kila maamuzi unayofanya, kila neno unalotamka na kila wazo unalowaza. unamheshimu Mungu unapochagua furaha ya uwepo wake. Humtukuzi Mungu kwa kunung'unika, kulalamika, kuwa na uchungu au kutokusamehe.

Unamtukuza Mungu unapochagua kukaidi magumu kwa furaha! Unahitaji ushauri wa roho mtakatifu na kuazimia kuwa hakika utafurahi pindi utakapokuwa unapitia magumu. Mistari hii inatufundisha kwamba hatutakiwa kuogopa mishale mikali... bali tunachotakiwa kufanya ni kufurahi!
siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com