Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 19 YA 31

Mfalme Daudi alijua umuhimu wa kuiambia nafsi yake kumbariki Bwana! Nafsi yako ni mahali pa mazalia ya hisia na hamu zako na kwa bahati mbaya nafsi yako siku zote "haijisikii" kama kumbariki Bwana. Kutakuwa na wakati katika maisha yako nafsi yako itatamani kulia na kutaka haki yake kusikiwa. Nyakati kama hizo ni lazima uifanyie kama unavyomfanyia mtoto wa miaka miwili ambaye umeshindwa kumdhibiti! Lazima uiamuru nafsi yako, kama Daudi alivyofanya, kumbariki Bwana.

Roho yako lazima iwe sehemu ya mtu wa ndani anayefanya mambo katika maisha. Bahati mbaya, katika karne hii ya 21, ya ulimwengu wa maarifa, tunaangalia sana nafsi kuliko roho. Hutaweza kuenenda kwa imani na wala si kwa kuona kama utaruhusu nafsi yako kukuongoza. Nafsi zetu zinaongozwa na mazingira lakini roho huongozwa na roho wa Mungu na neno la Mungu. Usiruhusu nafsi yako kuwa kiongozi wa roho yako hata kama itapiga kelele kiasi gani.

Nafsi yako inasema maneno ya huruma kama haya:

"Muziki huu unakelele sana. Nitakaa hapa na kuponda tuu"

"Nimechoka sana hata siwezi kunyanyua mikono yangu kuabudu."

" Siwezi kuweka chochote kwenye chombo cha sadaka juma hili."

"Nimechoka sana sieezi kwenda kwenye mafunzo ya Biblia. Kichwa kinaniuma. Yawezekana na uvimbe kichwani."

Wakati roho anaongea, hata hivyo, inakuwa kama neno la Mungu!

" Napenda kutoa kwa furaha!"

"Nakataa kuwa na mashaka.... nitamtumaini Bwana kuwa atanipa!"

"Nashukuru sana kwamba kanisa hili linaabudu kwa shauku!"

Kunja misuli yako ya kiroho na uruhusu roho yako ikuongoze na kulinda muitikio wa nafsi yako katika maisha.
siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com