Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 18 YA 31

Ni kitu gani roho yako inatamani? Unatamani kupata fedha nyingi? Unatamani kumwambia Mume wako mapenzi ndiyo basi? Unatamani kulala usiku mzima? Unatamani kuishi unavyotaka au kujieleza kwa uhuru bila kujizuia? Mtunga Zaburi alitamani kuwa nyuani mwa Bwana! Daudi alitamani kukaa nyuani mwake na kukaa na Bwana tuu katika utulivu wa uwepo wa Bwana.
Hutapata furaha ile iliyokusudiwa kwa ajili yako hata siku moja, mpaka utakapotatua hili suala la kutamani katika maisha yako. Utakapokuwa angalau unatamani uwepo wa Bwana na kufanya atakavyo na siyo utakavyo, ni wakati huo utakapo pokea furaha yake. Ni pale utakapotambua kwamba maisha yako si kuhusu wewe... ila ni kuhusu Yeye.... ndipo utakapopata utoshelevu wa furaha ipatikanayo tu katika uwepo wake. Matamanio ya haraka ya moyo wako ni kufurahi katika Yeye pekee.

Natumaini umepata utoshelevu wa ajabu unaotokana na kuimba wimbo wa sifa kwa Mungu. Wakati mwingine" utakapojisikia": kama kupasuka kwa hasira ... imba wimbo wa sifa badala yake. Siku nyingine "ukijisikia" kama kuelezea hadithi yako... unaonaje kama utainamisha kichwa chako na kuruhusu maneno ya tenzi yalete amani moyoni mwako? Siku nyingine ukidhihakiwa na msichana kazini kwako... kwa nini usigune wimbo wa sifa?
Panga upya majibunyako kutoka majibu ya hasira na kuwa wimbo... kutoka kwenye kuchanganyikiwa na kuwa wimbo wa kuabudu... na kutoka kutokuwa na subira na kuwa wimbo wa sifa. Mungu anajali sana majibu yetu tunavyokabiliana na masuala haya ya maisha yetu na mimi kama mtunga Zaburi wa kale, nachagua kuimba sifa!
siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com