Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 17 YA 31

Hakujatokea katika kumbu kumbu za historia jeshi lililokuwa limejiandaa kama la Yehoshafati katika nchi ya Yuda. Walimtazama Bwana! Walidumu katika nyumba ya Bwana! Walifunga na kuomba! Walianguka kifudifudi kumwabudu Bwana! Walipiga kelele za ushindi hata kabla vita haijaanza!

Wakati watu chini ya utawala wa Yehoshafati walikuwa wakiimba na kusifu, Mungu alikuwa anawapigania. Kanuni za Mungu hazibadiliki kama utatumia maisha yako kuimba na kusifu, Mungu atafanya kazi ya kukupigania. Je, unaamini hilo? Kama unaamini, utatumia muda wako mwingi kuabudu na muda mchache kuhofia. Kama kweli unaamini kanuni hii kutoka katika kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati, utatumia muda wako mwingi katika kusifu kuliko kusengenya.

Tunapofuata kanuni za Mungu jinsi zinavyopatikana katika Biblia, siku zote tutakuwa zaidi ya washindi kwa kuwa tunamtumikia Mungu ambaye siku zote hutuongoza kwenye ushindi.

Watu katika taifa hili lililozungukwa na maadui walitumia siku tatu wakikusanya nyara na hata hivyo zilikuwa zaidi ya uwezo wao wa kubeba. Mungu ni mwingi wa rehema kwa wale wanaoliitia jina lake katika hali za kukatisha tamaa za maisha yao. Siku zote Mungu atafanya zaidi ya maombi na matarajio ya watu wake tunapochagua kumwabudu kuliko kulia.

Watu walirudi Yerusalemu kwa furaha... walipata amani ya jabu... na Mungu akawapa kupumzika kutoka pande zote. Kulikuwa na furaha izidio baada ya hapo, sivyo?!
siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com