Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 15 YA 31

Yeshoshafati alifanya maamuzi mawili ya hekima katika kifungu hiki cha maandiko. Tunahitaji kuyaona maamuzi katika maisha ya huyu mtawala kijana ili kwamba, hata sisi pia, tuweze kushinda kila vita ambayo adui anatuingiza.

Kwanza kabisa, Yehoshafati atafuta msaada kutoka kwa Bwana! Hakwenda kwa rafiki zake... angalia kwenye google kitu ambacho Oprah alisema kuhusu hili... hakuweka taarifa hiyo kwenye mtandao wa facebook juu ya yale aliyokuwa anayapitia au anakabiliana nayo... au kuweka kwenye gazeti la New York Times. Yehoshafati alimwendea Bwana alipokuwa anakabiliwa na adui na wewe unatakiwa kufanya hivyo.

Tunafanyaje basi? Tunakwenda kwenye neno la Mungu na vita vyetu. Kama vita yako ni msongo wa mawazo, basi angalia Biblia inasemaje kuhusu msongo wa mawazo na kuhusu furaha. Kama uko kwenye vita ya magonjwa, angalia katika itifaki ya biblia na usome maandiko yote yanayohusiana na uponyaji na maombi unayoweza kuyaona humo. Kama unakabiliwa na madeni makubwa, angalia Biblia inasema nini juu ya upaji wa Mungu, utoaji na fungu la kumi.
Uamuzi wa pili ambao mfalme Yehoshafati alifanya ni alikaa nyumbani mwa Bwana. Usiache vita yako ikutoe nje ya kanisa au nje ya ushirika wa watu wa Mungu! Wakristo wengi kwenda kanisani wanapokuwa na msongo wa mawazo, au wanapoumwa. Unahitajinkuwa nyumbani mwa Bwana ili uweze kupigana vita yako kwa namna ya kimungu!
Kama shauku yako ni kuwa mkristo aliyejawa na nguvu za furaha ya mbinguni, basi maisha yako yanatakiwa yafanane na maisha ya Yehoshafati na utatafuta majibu kwenye neno la Mungu. Na pia, kama Yehoshafati, utafurahia uwepo wa Mungu unaopatikana nyumbani mwa Mungu.
siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com