Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 14 YA 31

Yehoshafati alikuwa mmoja watu wazuri wa kizazi chake. Alikuwa tayari kuleta mabadiliko katika ufalme wake na kuleta haki. Yehoshafati, kama mtu wa Mungu, aliwatia moyo watu chini ya utawala wake kumcha na kumtumikia Mungu kwa mioyo yao yote. Mmmmh natamani tungempata kiongozi wa namna hii leo!

Yehoshafati alikuwa akifanya mambo sahihi na kuishi maisha ya uadilifu na malengo! Alipofushwa na maadui walioikabili nchi yake na kuleta vita katika ufalme wake wenye amani. Ujasiri wa hawa maadui!

Ujasiri wa maadui zako pia! Wote tunakabiliwa na maadui wenye nguvu na tunaweza kuifunza somo moja ama mawili kutoka kwa mfalme kijana Yehoshafati. Yehoshafati alielekeza macho yake katika kumtafuta Bwana. Hakupoteza muda dakika hata moja kwa kuhofu au kumlaumu Mungu. Yehoshafati aliazimia kwamba macho yake yatamwelekea Bwana pasipokujali kwamba maadui walikuwa wanaelekea kwenye mipaka ya Yuda.

Ukitaka kushinda vita furaha, utayaelekeza macho yako kwa Bwana. Hutapoteza muda kuwa na hofu wala mashaka. Utaazimia moyoni mwako kwamba Bwana anahitaji usikivu wako pasipokujali yanayotokea kwenye mazingira yako.

Mara nyingi tunapokuwa katika vita, yote tunayozungumza ni vita tuu.... saratani... kutokuwa na fedha... gubu la mama mkwe... uasi wa mtoto. Zungumza habari za Bwana uwapo vitani! Chagua andiko na ulisimamie hilo!
siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com