Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 13 YA 31

Kwani furaha ni nini? Je, kuna fasili ya neno moja linaloweza kuelezea uzito wa neno hili rahisi na la muujiza? Sidhani... lakini yawezekana kuna maana nyingi zinazopatikana kwenye neno la Mungu kwa ajili ya neno hili lenye nguvu linaloleta tofauti katika maisha ya mkristo!

Furaha ni amani ipitayo ufahamu.

Furaha ni winginwa mashahidi wanaokushangilia kwa sauti kubwa!

Furaha ni ufahamu wa kwamba hakuna kitakachokutenganisha na upendo wa Mungu.

Furaha ni kutembea juu ya maji! Kama Petro!

Furaha ni kugeuza maji kuwa divai na kulisha maelfu ya watu kwa chakula kidogo kilichotolewa na kijana mdogo mkarimu.

Furaha ni malaika walio kilimani juu ya Bethlehemu usiku wenye nyota.

Furaha ni ukubwa wa mbegu ya haradali.

Furaha ni watoto.. wa aina zote na umri wote.. walioketi miguuni pa mtu wampendae wanayemwita, "Mwalimu".

Furaha ni kundi la nguruwe wanaokilimbilia kwenye maji na kuzama!

Furaha ni msichana bikira anayemwambia malaika " Na iwe kwangu kulingana na neno."

Furaha ni mtoto unapokuwa na umri wa miaka 90!

Furaha ni kijito jangwani na njia nyikani.

Furaha ni uwepo wake wa kimuujiza na usioisha hamu katika maisha yangu ya kawaida.
siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com