Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Watanzania wengi wametolewa mapepo kwa jina la Yesu. Kwa hiyo tunahitaji kwa umakini sana kuyaangalia mafundisho ya Yesu katika m.43-45: Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.Maana hapa anatuonyesha umuhimu wa kumtunza kiroho mtu wa namna hiyo. Huduma yetu haina maana ikiwa mtu amesaidiwa kwa siku moja, wiki moja au mwaka mmoja tu. Asiposaidiwa kiasi cha kuweza kusimama imara katika Yesu na kufika mbinguni hatujafanikiwa huduma yetu. Kuna utupu katika moyo wa mtu baada ya kutolewa pepo. Ni lazima utupu huu ujazwe na Neno la Mungu na sala!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz