Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Yohana Mbatizaji ni nabii wa mwisho wa Agano la Kale tena ni mkuu kuliko manabii wengine kwa sababu amepewa wajibu wa pekee wa kumtengenezea Bwana mwenyewe njia. Kazi ya Yohana ilileta uamsho mkubwa kwa Wayahudi, watu walimjia kwa wingi. Rudia m.12: Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Lakini pamoja na Yesu yanaanza majira mapya ambayo ni kutimizwa kwa maneno yote ya manabii. Ni majira ya kukaribia kwetu ufalme wa Mungu. Aliye mdogo katika ufalme wa Mungu, maana yake ni wanafunzi wa Yesu. Linganisha na Mt 10:42:Mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake. Wao ni wakubwa kuliko Yohana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz