Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Mungu ameitenga siku moja kwa ajili ya kupumzika na kuabudu. Kwa Wayahudi ilikuwa ni Jumamosi. Kwetu Wakristo imekuwa ni Jumapili tangu wakati wa mitume. Walichagua siku hii iwe sabato yao kwa sababu Jumapili ni siku ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu. Kusudi la Mungu kutupa sheria hii ni kutulinda na kututendea mema. Kwa hiyo Yesu alisali kwa uaminifu siku hiyo, kama ilivyoandikwa katika Lk 4:16, Siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake Pia alitumia siku hiyo kwa ajili ya kuwatendea mema walio karibu naye (ling. m.1: Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala- na Yesu anavyosema katika m.7, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia). Vivyo hivyo Yesu aliwahurumia wenye mahitaji ya uponyaji: Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, ukawa mzima kama wa pili.Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote(m.13-15). Tumfuate!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz