Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Yesu anayatilia umuhimu sana maneno yetu, maana tusemayo hufunulia hali ya moyo wetu. Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake,Yesu anasema katika m.34. Tafakari pia Rum 10:9-10: Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Mafarisayo walinena maneno mabaya juu ya Yesu. Walidai kwamba hutoa pepo kwa nguvu ya Shetani. Hayo maneno yao yanaonyesha kwamba ndani ya mioyo yao ni wabaya, kama Yesu alivyosema katika m.34,Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya?Kipimo kingine cha hali ya mioyo yetu kinasomeka katika m.30 ambapo Yesu anasema, Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. Huwezi kusimama katikati. Ama ni pamoja na Yesu au ni kinyume! Je, wewe unakusanya pamoja naye, yaani unawapenda walio wake na kuwavuta wengine kwake?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz