Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Yesu anafundisha juu ya jambo moja ambalo kwa kawaida hukosekana kwa sisi wanadamu, yaani unyenyekevu wa moyo mbele ya Mungu. Lakini bila huu hatuwezi kumtambua Mungu na Mwana wake Yesu Kristo. Yesu hujiweka mwenyewe kuwa mfano kwetu katika hili (m.29: Mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo. Flp 2:5-8 huonyesha hiyo ni kweli). Watoto wachangapia ni mfano (m.25:Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga). Watoto wachanga wanahitaji kupokea kila kitu, hawawezi kujisifia uwezo wo wote. Basi, sikia wito wa Yesu wa m.28 ukajinyenyekeze mbele yake!Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Hivyo utapata raha nafsini mwako (m.29).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz