Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

SIKU 23 YA 30

Neno hili laweza kutufundisha mambo mawili. Kwanza ni utii kwa neno litokalo kinywani mwa Mungu. Ijapokuwa marafiki waliomtaabisha Ayubu walimhuzunisha, Mungu alipomtaka Ayubu awaombee, Ayubu alitii. Utii kwa neno la Mungu ni sharti la Biblia. Jambo la pili ni kuwaombea waliotukosea. Hili nalo ni takwa la kimungu na kutusaidia kushinda mafarakano. Zingatia Lk 6:27-28: Nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,  wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Mambo haya mawili yalikuwa msingi wa Ayubu kurejeshewa ufanisi, uliokuwa umepotea. Kumbuka mambo haya na kuyaishi siku zote.

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz