Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Kitabu cha Ayubu ni simulizi ndefu ambapo Ayubu alipatwa na mateso mengi. Wakati alipokuwa akiteseka, marafiki zake, Elifazi na wenzake watatu, walimtuhumu Ayubu kwamba alikuwa anapata taabu kwa sababu alikuwa mdhambi. Hawakufahamu kuwa mapito ya Ayubu yalikuwa ni kusudi la Mungu. Ni rahisi kuwahukumu wenzetu kwa jambo lisilo sahihi. Biblia yafundisha: Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi. Soma Mt 7:1-5 kwa ufafanuzi mpana zaidi: Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.Tuwahurumie wenzetu na kuwaombea katika dhiki zao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz