Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Somo hili linatupa picha ya safari ya Yesu kuelekea msalabani. Yale maumivu yote aliyoyapitia hapo (m.3-9) ni maandalizi ya kutufanyia uponyaji wa uhusiano wetu na Mungu. Ilibidi Yesu apitie taabu hii ya nafsi, mwili na roho ili sisi tuwe na kimbilio. Kwa njia hiyo Mungu alikamilisha kusudi la mapenzi yake, ambayo ni kuwafanya wengi kuwa wenye haki (m.11). Mlolongo huu wa matukio huleta maumivu makali ya moyoni, lakini pia huleta furaha kubwa na shukrani kwa Mungu. Yesu ndiye kafara iliyotuokoa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz