Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Mambo yote yaliyotabiriwa kuhusu Yesu, hata aina ya kaburi alimozikwa yalitimia na yameendelea kudhihirika hata leo. Isaya 53:9 inasema: Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.Mstari huu ulitimia katika kifo chake kilicholeta wokovu. Ijapokuwa Yesu alidharauliwa na kudhalilishwa, heshima na ufalme wake uliendelea na unaendelea kudhihirika kwa watu wote. Kwa hiyo hakuna nguvu wala mamlaka itakayoweza kuuzuia au kuufunika ukuu wa Yesu. Yeye ataadhimishwa katika maeneo yote ya maisha yetu. Kwa sababu hiyo, astahili kuwa Bwana wetu sisi sote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz