Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

SIKU 15 YA 30

Maneno haya ni 'faraja' ya Elifazi kwa Ayubu. Anamhesabu kuwa mwovu astahiliye hasira ya Mungu. Lakini ijapokuwa Elifazi hakuelewa kisa cha mateso ya Ayubu, maneno yake yanabeba mafundisho muhimu kwetu. Mwovu anaweza kupata mafanikio, lakini hatakuwa tajiri, wala mali zake hazitadumu(m.29a). Ustawi wake ni wa kitambo tu, na hatimaye ataishia kwenye maangamizi (ukitaka kujifunza zaidi kuhusu hatima ya mwovu, soma Kum 28:15-68). Heri tusitumainie ubatili (m.31, Asiutumainie ubatili, na kujidanganya; kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake). Kumwishia Mungu katika uadilifu ni njia ya mwisho mwema.

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz