Soma Biblia Kila Siku 04/2020Mfano
Leo tunafundishwa habari za kutembea na Yesu Kristo aliyefufuka. Yesu alijiunga na Kleopa na rafikaye pasipo wao kumtambua walipokuwa safarini. Kisha akaingia na kujifunua kwao katika kuumega mkate. Yesu yu hai. Yupo mlangoni anagonga daima (Ufu 3:20, Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami). Fungua mlango wa maisha yako umkaribishe. Baraka ya kutembea naye ni kutembea nuruni. Yesu ni nuru ya ulimwengu. Tena Yesu hutupa nguvu kupeleka Habari Njema kwa wengine, kama kina Kleopa walivyopeleka habari za kufufuka kwa Yesu Yerusalemu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz