Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 14 YA 30

Musa anapanda mlima Nebo ili afie huko, kama alivyoambiwa na Bwana, Kwea katika mlima huu wa Abarimu, mpaka kilima cha Nebo, kilicho katika nchi ya Moabu, kuelekea Yeriko; ukaangalie nchi ya Kanaani niwapayo wana wa Israeli kuimiliki; ukafe katika kilima, huko ukweako, ukusanywe uwe pamoja na jamaa zako; kama alivyokufa nduguyo Haruni katika mlima wa Hori, akakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa sababu mlinikosa ninyi juu yangu katikati ya wana wa Israeli katika maji ya Meriba huko Kadeshi, katika bara ya Sini; kwa kuwa hamkunitakasa katikati ya wana wa Israeli. Kwani utaiona hiyo nchi mbele yako, lakini hutakwenda huko kuingia hiyo nchi niwapayo wana wa Israeli(Kum 32:49-52). Kabla Musa hajafa, Bwana anatimiza ahadi yake na kumwonyesha nchi nzima ya Kaanani (m.1: Bwana akamwonyesha nchi yote). Baadaye Musa akafa akiwa na miaka 120. Kama ilivyoandikwa katika m.5-6, Bwana mwenyewe alimzika, na kaburi lake halitambulikani (ling. Yud 1:9, Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee). Inasisitizwa kuwa hakuna nabii mkubwa kama Musa aliyeinuka tena katika Israeli: Hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso(m.10). Bwana alikuwa anaongea naye kwa njia ya kipekee, kama anavyoeleza katika Hes 12:6-8,Sikizeni basi maneno yangu; akiwapo nabii kati yenu, mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; kwake nitanena mdomo kwa mdomo, maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?Kristo peke yake ni mkuu kuliko Musa, maana amemfunua Mungu kwa ukamilifu akiwa Mwana wake: Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua(Yn 1:18). 

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz