Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Kwa mstari wa 15-16 Paulo anaonyesha kuwa msukumo wake wa kutaka sana kuwatembelea Wakristo wa Rumi ni Injili yenyewe: Mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi. Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Kuijua Injili, yaani habari njema ya Yesu Kristo, ni utajiri mkubwa kupita kiwango! Maana Injili ina uwezo wa kufanya jambo la ajabu ambalo hakuna kitu kingine duniani kinachoweza kulifanya, yaani inaweza kumwokoa mwanadamu! Haki ya Mungu inadhihirishwa ndani ya Injili, toka imani hata imani(m.17). Yaani kwa kuaminimatendo ya wokovu ya Yesu Kristo, mtu huhesabiwa kuwa mwenye haki mbele ya Mungu! Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo (Efe 2:8-9).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila Asubuhi

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021
