Soma Biblia Kila Siku 9Mfano
Pauloakijitambulisha kama mtumwa wa Kristo Yesu(m.1), maana ya "mtumwa" ni kwamba amejiweka chini ya mapenzi ya Yesu Kristo kwa kila jambo la maisha yake! Je, wewe umefanya hivyo? Hii ni barua ya msingi kutoka kwa mtume Paulo. Humo amepanga kwa utaratibu mafundisho ya msingi juu ya imani ya Kikristo. Ina sehemu kuu mbili: 1. Imani ya Mkristo (1:18-11:36). 2.Matendo ya Mkristo (12:1-15:33). Paulo anahubiri Injili ya Mungu(m.1), ambayo ni habari njema inayomhusu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kristo ametajwa mara 7 katika mistari hii 7 ya kwanza!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz