Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 20 YA 30

Kama inavyoonekana katika m.12 na 17, Paulo aliwalenga Wayahudi kwa maneno ya somo hili: Wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria. ... Wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati …. Wengi wao walimkataa Kristo kwa sababu walikuwa wameambukizwa na unafiki wa Mafarisayo (Mt 23:1-7 na 23-28 inaeleza zaidi kuhusu unafiki huu). Mtu anaweza kwa mwenendo wake kuonekana mwema sana kuliko wale waliozungumziwa katika Rum 1:18-32. Ila haitamsaidia lo lote ikiwa kwa siri huyatenda yale yale, na kwa moyo wake yuko mbali na Mungu. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa(Mt 7:2). Mungu hana upendeleo. Hutafuta moyo ulio na toba ya kweli.Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? (m.4). Je, una roho gani? Roho ya uasi na unafiki au roho ya toba?

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz