Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 25 YA 30

Kwa sababu hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake [Mungu], lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu(Ebr 4:13), Paulo anaweza kuonyesha jinsi kila binadamu anavyoonekana machoni pa Mungu. Huenda machoni pa watu wengine na hata machoni petu wenyewe tunaonekana watu wema. Lakini kwa Mungu sivyo. Kumcha Mungu hakupo machoni pao (m.18). Maana Mungu anadai ukamilifu! Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote (Mt 22:37).Ukamilifu huu hajauona kwa mtu ye yote (m.10-12: Hakuna mwenye haki hata mmoja.Hakuna afahamuye; hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; hakuna mtenda mema, la! hata mmoja). Kwa hiyo njia ya kuokolewa ni kwa neema ya Mungu tu. Kwa kupewa sheria, Wayahudi walisaidiwa sana kutambua hali hiyo: Mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;  kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria (m.19-20).

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz