Soma Biblia Kila Siku 9Mfano
Somo hili lafunua kwa sehemu maana ya Utatu wa Mungu. Kabla haijawako dunia, alikuwepo Mungu peke yake – Hekima akiwa pamoja naye! Rudia m.22-23 na 30 ukizingatia ina maana gani, Hekima anaposema: Bwana alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, kabla ya matendo yake ya kale.nalitukuka tokea milele, tangu awali, kabla haijawako dunia. ... Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; nikawa furaha yake kila siku; nikifurahi daima mbele zake.Wakristo wa nyakati zote wameona fungu hili linatupa picha halisi ya uhusiano wa Yesu na Mungu Baba. Tangu milele Yesu alikuwako na kutukuka.Alikuwa ni lile tamkola Mungu katika uumbaji (Yn 1:3: Vyote vilifanyika kwa huyo [Neno]; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika). Tena Yesu yu ndani ya Baba, na Baba yu ndani ya Yesu. Katika Yn 14:10-11 Yesu anasema, Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu. Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu. Kwa hiyo twamwadhimisha Yesu sawa na Baba (na pia Roho Mtakatifu).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz