Soma Biblia Kila Siku 9Mfano
Hapananjia ya katikati ya kuweza kushinda kesi yako mbele ya Mungu. Njia ya katikati ni kule kujisifia matendo yako mema mbele ya Mungu pamoja na kumwomba kwa neema yake akusamehe pale ulipokosa na kupungukiwa. Kwenye njia hii hakuna neema kabisa! Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu (m.2). Kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni (m.4). Ukitaka kwamba matendo yako yakusaidie kushinda kesi, ni lazima uwe mkamilifu kwa matendo, maneno na mawazo! Huwezi! Bali ukitambua hali yako ya upotevu na kukubali kuamini kuwa Mungu anataka kukusamehe bure kwa neema tu, hapo umeokoka! Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki(m.3). Kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki(m.5).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz