Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 22 YA 30

Katika m.1, Mungu anajiita Hekima, na pia Busara. Mungu hunena na watu kila mahali, si kwa njia ya mahubiri tu, bali hata kwa matendo yake ya kila siku yanayoonekana: Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake(Rum 1:19-20). Hayo ni sauti inayotuita tumheshimu na kumnyenyekea; na wamchao wanaelewa. Ukitafakari kwa umakini yote uyasikiayo na kuyaona, humo ndani yake utapata ujumbe wa Mungu unaokuelekeza umtukuze! Utakapotenda hilo, atakufunulia utajiri udumuo wa maarifa na busara zake. Matunda yake ni haki na heshima (m.18-19: Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, Na faida yangu hupita fedha iliyo teule).

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz