Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 18 YA 30

Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu(m.18). Kabla Paulo hajaendelea kufundisha zaidi juu ya Injili, anatumia nafasi ya kuonyesha jinsi Mataifa (1:18-32) na Wayahudi (2:1-3:20) wanavyopotea na kuhukumiwa na ghadhabu ya Mungu. Kuna makosa mawili ya msingi yanayomtenganisha Mtaifa na Mungu: 1. "Uasi", yaani kutokumwamini na kumtukuza Mungu (m.21-23:Walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo). 2."Uovu", yaani kufanya yasiyo haki. Ndivyo wanavyofanya waipingao kweli kwa uovu (m.18). Je, uko chini ya ghadhabu ya Mungu?

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz