INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJAMfano
MEZA YA BWANA
MATTHEW 26
Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu wanafunzi walimjia Yesu wakamwuliza,
“Unataka tuandae wapi kwa ajili yako ili kuila Pasaka?”
Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia, nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’
Hivyo wanafunzi wakafanya kama vile Yesu, alivyokuwa amewaelekeza, nao wakaandaa Pasaka.
Ilipofika jioni, Yesu alikuwa ameketi mezani pamoja na wale kumi na wawili.
JOHN 13
Hivyo aliondoka chakulani, akavua vazi lake la nje, akajifunga kitambaa kiunoni.
Kisha akamimina maji kwenye sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni.
Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, je, wewe utaninawisha mimi miguu?”
Yesu akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.”
Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.”
Yesu akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.”
Ndipo Simoni Petro akajibu, “Usininawishe miguu peke yake, bali pamoja na mikono na kichwa pia!”
Yesu akamjibu, “Mtu aliyekwisha kuoga anahitaji kunawa miguu tu, kwani mwili wake wote ni safi. Ninyi ni safi, ingawa si kila mmoja wenu.”
Kwa kuwa yeye alijua ni nani ambaye angemsaliti, ndiyo sababu akasema si kila mmoja aliyekuwa safi.
Alipomaliza kuwanawisha miguu yao, alivaa tena mavazi yake, akarudi alikokuwa ameketi, akawauliza,
“Je, mmeelewa nililowafanyia? Ninyi mnaniita mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana,’ hii ni sawa, maana ndivyo nilivyo."
Kwa hiyo, ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi.
Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi.
Baada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”
Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. "Mmoja wa wanafunzi wake, ambaye Yesu alimpenda sana alikuwa ameegama kifuani mwa Yesu.Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi akamwambia, “Mwulize anamaanisha ni nani.”
Yule mwanafunzi akiwa amemwegemea Yesu akamwuliza,“Bwana tuambie ni nani?”
Yesu akajibu, “Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya kwenye bakuli.”
Hivyo baada ya kukichovya kile kipande cha mkate, akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.
"Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, Shetani akamwingia.Yesu akamwambia Yuda,"
“Lile unalotaka kulitenda litende haraka.”
"Hakuna hata mmoja wa wale waliokuwa ameketi nao chakulani aliyeelewa kwa nini Yesu alimwambia hivyo.Kwa kuwa Yuda alikuwa mtunza fedha, wengine walifikiri Yesu alikuwa amemwambia akanunue vitu vilivyohitajika kwa ajili ya Sikukuu, au kuwapa maskini cho chote."
Mara tu baada ya kupokea ule mkate, Yuda akatoka nje. Wakati huo ulikuwa ni usiku.
MATTHEW 26
Kisha Yesu akawaambia, “Usiku wa leo ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa:
‘Nitampiga mchungaji,nao kondoo wa hilo kundi watatawanyika.’Lakini baada ya mimi kufufuka, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
Petro akajibu “Hata kama wote watakuacha, kamwe mimi sitakuacha.”
Yesu akajibu, “Amin, amin ninakuambia,
usiku huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Lakini Petro akasema,
“Hata kama itabidi kufa pamoja na wewe, kamwe sitakukana.”
Nao wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.
MARK 14
Walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega
na kuwapa wanafunzi wake akisema, “Twaeni mle, huu ndio mwili wangu.”
Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa wanafunzi wake, wote wakanywa kutoka humo.
Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.
Amin nawaambia, sitakunywa tena uzao wa mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika Ufalme wa Mungu.”
Amin nawaambia, sitakunywa tena uzao wa mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika Ufalme wa Mungu
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org