INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJAMfano
HUKUMU
“Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu wake.Mataifa yote watakusanyika mbele zake,
"naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi.Atawaweka kondoo upande wake wa kuume na mbuzi upande wake wa kushoto."
“Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wake wa kuume, ‘Njoni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha,
nilikuwa uchi mkanivika, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.’
“Ndipo wale wenye haki watakapomjibu wakisema, ‘Bwana, ni lini tulikuona una njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakunywesha?Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukiwa uchi tukakuvika?Tena ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukakutunza au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’
“Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin, amin ninawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.’
Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa,
nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake.
Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu hamkuninywesha,
nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha,
nilikuwa uchi hamkunivika, nilikuwa mgonjwa hamkunitunza na nilikuwa gerezani nanyi hamkuja kunitembelea.’
“Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au uchi, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’
“Naye atawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’
Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org