INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJAMfano
SADAKA YA MJANE MASKINI
"Kisha Yesu akaketi mkabala na sehemu sadaka zilikokuwa zinawekwa na kuangalia umati wa watu wakati wakitoa fedha zao kwenye hazina ya Hekalu. Matajiri wengi wakaweka kiasi kikubwa cha fedha.Lakini mjane mmoja maskini akaja na kuweka sarafu mbili ndogo za shaba zenye thamani ya senti mbili.Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia,
“Amin, amin, nawaambia, huyu mjane maskini ametoa zaidi katika hazina kuliko wengine wote.Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mjane kutokana na umaskini wake, ametoa kila kitu alichokuwa nacho, hata kile alichohitaji ili kuishi.”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org