Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJAMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJA

SIKU 5 YA 7

  

KUTAWADHA MIGUU YA YESU

Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi.

Wakaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu.

Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja safi ya thamani kubwa akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,

“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300 na fedha hizo wakapewa maskini?”

Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwivi, kwani ndiye aliyekuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

Yesu akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu.Maskini mnao siku zote lakini mimi hamko pamoja nami siku zote.”

"Alipomiminia haya manukato kwenye mwili amefanya hivyo ili kuniandaa kwa ajili ya maziko yangu.Ninawaambia kweli, mahali po pote habari njema itakapohubiriwa ulimwenguni mwote, jambo hili alilofanya litatajwa pia, kwa ukumbusho wake.”

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More

Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org