Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJAMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJA

SIKU 2 YA 7

  

MFANO WA WANAWALI KUMI

“Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi.Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara."

"Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo."

Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.

“Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!" 

“Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao.Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo, taa zetu zinazimika."

“Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’

“Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari, wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.

“Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’“Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’

“Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More

Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org