Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
“Mtu astahiliye kudharauliwa” hufafanuliwa kuwa sawa na ‘pembe ndogo’ katika maono ya Danieli (8:9-27), yaani ni unabii kuhusu Antioko Epifani aliyetawala mwaka 175-164 k.K. Alinajisi hekalu la Yerusalemu kwa kuweka sanamu ya mungu wake mahali pa madhabahu ya Bwana (m.31: Wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu), na ni mtangulizi wa mpinga Kristo. Wamjuao Mungu, ndio wale tu watakaosimama imara wakati huu wa majaribu na mateso. Hata baadhi yao watauawa. Lakini angalia, hakuna kinachotendeka bila kuamriwa na Mungu (m.27: Katika habari za wafalme hao wawili, mioyo yao watanuia kutenda madhara, nao watasema uongo walipo pamoja mezani; lakini hilo halitafanikiwa; maana mwisho utatokea wakati ulioamriwa. M.35: Na baadhi yao wenye hekima wataanguka, ili kuwatakasa, na kuwasafisha, na kuwafanya weupe, hata wakati wa mwisho; kwa maana ni kwa wakati ulioamriwa, ambao haujaja)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz