Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 7](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F15759%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Agabo ... akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa(m.10-11). Neno hili halikumfanya Paulo kuogopa wala kuahirisha safari yake ya kwenda Yerusalemu. Bali lilikuwa kwake thibitisho ya kwamba haya ndiyo mapenzi ya Bwana. Linganisha na 20:23 anaposema: Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. ... Nao [Wakristo wa Tiro]wakamwambia Paulo kwa uweza wa Roho asipande kwenda Yerusalemu (21:4). Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu. Alipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na yatendeke(21:13-14). Kanisa la kwanza lilikuwa na wenye karama ya kutabiri mambo yajayo (angalia tena m.4, na m.9: Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri. Linganisha na 11:27-28, Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia. Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio). Ni muhimu sana kupima unabii. Ukitaka kujua zaidi jinsi ya kuupima, soma Kum 18:21-22; 1 Kor 14:29 na Efe 2:20.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 7](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F15759%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz