Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Wayahudi waliotoka Asia (m.27). Katika ulimwengu wakati ule (mwaka 58 B.K.) Wayahudi wengi walikuwa hawakai katika nchi yao wenyewe bali walikuwa wametawanyika katika nchi nyingi. Hata hivyo walihesabu Yerusalemu kuwa ni mji wao mkuu na mtakatifu kwa sababu ya hekalu kuwepo hapo. Hivyo wenye uwezo walijitahidi kusafiri kwenda Yerusalemu mara kwa mara hasa wakati wa sikukuu ili kuabudu na kuona ndugu. Lugha ya Kiebrania(m.40) ni lugha yao wenyewe Wayahudi. Mwondoe huyu (m.36). Ndivyo Wayahudi walivyosema kuhusu Yesu: Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu (Lk 23:18). Yesu mwenyewe alitabiri itatokea hivyo:Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka(Yn 15:20-21).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz