Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Miguuni pa Gamalieli(m.3). Huyu mzee ni mwalimu aliyeheshimika sana: Mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru... (Mdo 5:34). Ni yeye aliyetoa ushauri kwa viongozi wa Wayahudi kwamba wawaache Petro na Yohana ili baraza lisije likapinganana Mungu: Nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu(5:38-39). Ila Paulo alikuwa mkali kuliko mwalimu wake: nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua(m.4). Katika upofu wake wa kiroho alikuwa akifikiri kuwa kwa njia hiyo humtumikia Mungu! Ila sasa anashuhudia jinsi Yesu aliye hai alivyomwokoa. Je, unasikia wito wa m.16? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake [Yesu]. Je, ni jina gani unaloliitia moyoni mwako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz