Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 7](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F15759%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Watu walio na uelewa mzuri wa mahusiano yampasayo mwanadamu na Muumba wake, hulindwa dhidi ya uovu, ili wasiharibikiwe nao. Ukijiamini tu, uovu utakuteka. Mfano ni jinsi kahaba amvutiavyo mwanamume kwa maneno ya ulaghai hata akaipoteza njia adili. Hao wataangamia kwa pamoja. Kufunga ndoa ni kufanya agano na wawili, nao ni mwenzako na Mungu. Hivyo uzinzi una matokeo mabaya sana: Amwendeaye kahaba harudii tena njia ya uzima (m.17 na 19:Amwachaye rafiki wa ujana wake, Na kulisahau agano la Mungu wake.... Katika hao wamwendeao [mayala]harudi hata mmoja, Wala hawazifikilii njia za uzima). Ni wanyofu tu watakaoirithi nchi ya Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 7](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F15759%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz