Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano
“Anafanya Mambo Yote Kukupatia Mema”
Mungu anatawala maeneo yote ya maisha yetu. Ana uwezo wote wa kufanya hali yo yote kuleta faida kwetu kama waamini.
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” Warumi 8:28
Ana uwezo mkamilifu wa kushughulika na hata changamoto ngumu zaidi za maisha, na atatuongoza katika mapito ya kutimiza mpango Wake kwa maisha yetu. Anataka tu sisi kumtumaini Yeye kufanya hivyo.
“Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.” Mithali 3:5-6
Kuweka tumaini letu kwa Mungu haichukui nafasi ya wajibu binafsi na uwakili mwema. Isipokuwa, wajibu binafsi na kumtumaini Yeye vinakwenda sambamba. Tunapofanya sehemu yetu, Mungu siku zote ni mwaminifu kufanya sehemu yake na kutuongoza kikamilifu.
Mara nyingi, uongozi wa Mungu huja kwa njia ya "mlango" uliofunguliwa au kufungwa katika mazingira yetu. Wakati mwingine, hali zetu zinahitaji tu kuingilia kati kwa Mungu kwa hali yake ya Kiungu katika kuponya, kutenda muujiza au kukamilisha jambo fulani ambalo bila hivyo insigewezekana.
Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yanawezekana." Mathayo 19:26
Kwamba iwe ni kukabiliwa na ugonjwa usio na tiba, matatizo ya ki-fedha, au hata kuondokewa kwa kutotarajia kwa umpendaye, Mungu yupo na anaweza kutenda kiungu katika nyakati hizo.
Mungu ni mtaalamu wa kubadili msiba kuwa ushindi na tatizo kuwa furaha kupitia Roho Mtakatifu. Usiwe na wasi wasi Mungu bado yuko katika "shughuli ya kutenda miujiza" leo. Mungu anaweza kuingilia kati hali yo yote iliyoshindikana!
Kuhusu Mpango huu
Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2