Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

SIKU 2 YA 8

"Mungu   amekuja Kwako!”

Ahadi ya   uzima wa milele ni matokeo ya Mungu kuja kwetu na sio mwanadamu kujaribu   kumtafuta Mungu aliye mbali.

Tangu   mwanzo, Mungu amempenda kila mmoja wetu kwa upendo usio na sababu na unaodumu   millele. Nia yake katika mwanzo ilikuwa ni kuwa na uhusiano wenye  nguvu na ulio hai na kila mmoja wetu.   Lakini, mara Adamu na Hawa walipokosa utii kwa Mungu pale bustanini, dhambi   yao ikatengeneza kiambaza kati yetu na Mungu. Tukatengwa milele kutoka   Kwake.

Badala ya   kutuacha tuliotengwa na Yeye, Mungu akaanzisha mpango mkamilifu wa urejesho –   mpango unaosukumwa na upendo Wake usio na mwisho na rehema kwetu. Lengo la   mpango wake ni kurejesha kikamilifu uhusiano wa karibu kabisa na mwanadamu   kama ulivyokuwa kabla ya Adamu na Hawa hawajatenda dhambi.

Zaidi ya   miaka 2,000 iliyopita, Mungu alimtuma Mwanae ulimwenguni kuondoa kiambaza   kilichosababishwa na dhambi, na kufanya wokovu kupatikana kwa wote.

"Kwa   maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili   kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu   hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe   katika yeye.” Yohana 3:16-17

Kupitia   kifo na kufufuka kwake, Yesu alilipa malipo kamili kwa niaba yetu kwa adhabu   ya dhambi, na kuondoa kiambaza kati yetu na Mungu. Msamaha unapatikana kwa   wote walio tayari kumpokea Yeye kama Mwokozi wao.

Lakini hii ilikuwa ni mwanzo tu. Kabla Yesu hajamaliza   muda wake duniani kujumuika na Baba Yake Mbinguni, alifafanua kwa wanafunzi   wake sehemu nyingine ya mpango mpana wa Mungu wa kumrejesha mwanadamu   kikamilifu Kwake:

"Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama   sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na   kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi,   nanyi mwepo." Yohana 14:2-3

Sio tu kwamba Mungu alimtuma Yesu kuondoa kiambaza cha   dhambi, lakini siku moja huko mbeleni Yesu atarudi kuwachukua waamini wote   “”nyumbani”” kuwa Naye milele.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2