Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano
“Balozi wa Mbinguni – Roho Mtakatifu”
Balozi ni mwakilishi wa Kiserikali wa nchi moja kwenda nchi nyingine anayetumwa kuishi kati ya watu wa nchi hiyo, kutimiza utume wa amani na mahusiano mema. Anatimiza wajibu wake kwa mamlaka, ukarimu na na rasilimali za Serikali anayoiwakilisha. Kwa imani kubwa iliyowekwa juu yake, hutimiza kusudi lake kwa heshima kubwa hata kulikamilisha.
Katika njia nyingi, utume wa Roho Mtakatifu unafanana na kuwa balozi kutoka mbinguni. Roho Mtakatifu ana mamlaka yote, nguvu na rasilimali za Mungu, na anawakilisha na kuonyesha upendo wa Mungu kwa kila mtu katika ulimwengu kupitia uwepo na kazi zake.
Yesu alipokaribia kumaliza muda wake na wanafunzi, Aliwaambia kwamba hatawaacha peke yao atakapoondoka. Aliwaambia juu ya Mmoja atakayetumwa katika nafasi yake kuwa nao, kuwaongoza, kuwafundisha, kuwafariji na kuwaongoza – Roho Mtakatifu. Yesu alisema:
"Yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu." Yohana 16:7
Baada ya kazi ya Yesu duniani kukamilika, Alimpeleka Roho Mtakatifu kuwa pamoja nasi katika nafasi yake mpaka atakaporudi tena. Roho Mtakatifu anatoa uongozi, faraja na ushauri juu ya maisha yetu. Yesu alimwelezea Roho Mtakatifu kwa wanafunzi kwa jinsi hii:
"Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia." Yohana 14:26
Uwepo wa Mungu uko pamoja nasi leo kwa njia ya Roho Mtakatifu, na yu hai akifanya kazi katika ulimwengu wetu na maisha yetu.
Kuhusu Mpango huu
Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2