Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

SIKU 7 YA 8

“ Anajenga Tabia na Mwenendo Kukusaidia Wewe Kukua”

Tabia na   mwenendo mzuri si kitu tunachopokea pamoja na wokovu, lakini twajifunza na   kuukuza kadiri muda unavyoendelea. Kutusaidia sisi kujenga tabia ya Kristo ni   moja ya malengo ya msingi ya Mungu. Roho Mtakatifu hutusaidia sisi kufanana   zaidi na Yesu kwa kujenga na kuendeleza tabia yake ndani yetu. Biblia inaita   jambo hili Tunda la Roho.

“Lakini   tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili,   uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” Wagalatia   5:22-23 

Kati kati   ya changamoto, wakati mwingine tunajaribu kushinda matatizo kwa nguvu zetu   wenyewe. Kwa kufanya hivyo, tunaweza hata kujaribiwa kurahisisha tabia zetu   za Kikristo ili kupita katika magumu yanayotukabili, au  "kuchukua njia mkato." Lakini   tunapoiitia nguvu ya Roho Mtakatifu, Anatusaidia kukabili njia kwa uadilifu, kweli   na uaminifu, bila kujali mazingira.

Katika   wakati wa mafanikio, viwango vile vile vya Kibiblia vinapaswa kutawala. Kiburi na majivuno ni mambo ambayo yanapingana   moja kwa moja na tabia ya Kikristo Mungu anayotaka kuijenga katika maisha   yetu. Unyenyekevu ni hitaji la kila   Mkristo ili kuweza kuinuliwa na Mungu. 

"Heri   wenye upole; Maana hao watairithi nchi." Mathayo 5:5 

Tunapokabili   vyote, changamoto na mafanikio kwa tabia ya Kristo, tunaanza kukua katika   mwendo wetu na Mungu. Tunaaza hata kutambua kuwa kutenda katika Tunda la Roho   ni faida kwetu na heshima kwa Mungu. Tunavyozidi kukua katika mwendo wetu na   Mungu, ndivyo Mungu anavyozidi kuleta   baraka zake kubwa katika maisha yetu!

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2