Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

SIKU 5 YA 8

“Anafanya   Wokovu Kuwa Halisi kwa Mtu”

Wakati   ambapo ni Yesu ndiye aliyelipia wokovu wetu, ni uwepo wa Mungu kupitia Roho   Mtakatifu ndio unaofanya wokovu kuwa halisi kwa mtu kwa kila ambaye   ataupokea. Yesu aliweka wazi kwamba hatupokei wokovu  wakati tunapozaliwa. Kuna kuzaliwa kiroho   ambako lazima kutokee, hali ambayo Roho Mtakatifu pekee ndiye awezaye   kuisababisha.

Yesu   akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji (kuzaliwa kimwili)   na kwa Roho (kufanywa upya kiroho), hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.   Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa na Roho ni roho." Yohana   3:5-6

Mara mtu   anapompokea Kristo katika maisha yake, inahusisha kufanywa upya kiroho kwa   mtu wa ndani, inayoleta kuondolewa kabisa kwa adhabu ya dhambi katika maisha yake.

Pia, Roho   Mtakatifu yumo kazini katika maisha ya wasioamini kufunua upendo wa ajabu wa   Mungu kwa ajili yao. Yesu alisema,

"Lakini   ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli   atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia." Yohana 15:26

Leo, Roho   Mtakatifu anaendeleza huduma yake ya ajabu ya kufanya upendo wa Mungu   kujulikana kwa kumtangaza Yesu, aliye upendo binafsi wa Mungu, na yote   anayoyawakilisha kwa watu wote waamini na wasioamini ulimwenguni.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2