Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano
"Hauko Peke Yako”
Huwa inasemwa kwamba maisha yanahusisha mabonde na milima, wakati wa kufurahi na ahadi zilizojaa nyakati za changamoto na mashaka. Maisha sio kupanda kwenda kileleni juu siku zote; isipokuwa ni safari yenye milima na mabonde. Kila mmoja, waamini na wasioamini kwa pamoja, hupitia maisha ya kwenda juu na chini.
Lakini kama Wakristo, tuna ahadi ya ajabu toka kwa Mungu kwamba hatutakabili mabonde ya maisha peke yetu. Haya hapa maneno yake ya kutia moyo kwetu:
“Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.” Kumbukumbu la Torati 31:6
Ukweli ni kwamba tunahitaji uwepo wa Mungu katika nyakati zote za changamoto na nyakati za mafanikio. Kwa kujua Mungu yu pamoja nasi, tunaweza kukabili kila changamoto ya maisha kama ngazi kuelekea mafanikio na wala sio kushuka kuelekea kukata tamaa.
Hakuna mlima ulio mkubwa kupita kiasi au bonde lililo chini sana ambalo Mungu hatakutana nasi. Haijalishi mazingira yanayotukabili, Mungu ni mwaminifu, na siku zote yuko nasi!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2