Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano
“Utume wake ni kwa Mtu Binafsi”
Kutoka mwanzo wa uumbaji, Roho Mtakatifu amekuwepo, akikaa kati yetu kwa vizazi vyote.
“Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.” Mwanzo 1:2
Lakini ilihitaji mpaka Yesu kukamilisha kazi yake pale msalabani ndipo huduma ya Roho Mtakatifu kufanyika kuwa binafsi na nafsi ya karibu sana kwa kila mwamini. Yesu aliwaambia wanafunzi wake kabla hajafa kwamba Roho Mtakatifu yuko kati kati yao, lakini bado haishi ndani yao.
"Ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea (Roho Mtakatifu), kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu." Yohana 14:17-18
Ahadi ya Yesu ya faraja kwa wanafunzi wake kabla tu ya kifo chake ilikuwa kwamba bado atakuwa pamoja nao kiroho, kupitia uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha yao. Kazi Yesu aliyoanza inaendelea katika maisha yetu kupitia Roho Mtakatifu. Mungu anamtumia Roho Mtakatifu ndani yetu kufanya mambo manne:
1. Anafanya wokovu kuwa halisi kwa mtu.
2. Anakupa nguvu za kuishi kwa ushindi.
3. Anajenga tabia ya Kikristo kukusaidia kukua.
4. Anafanya mambo yote katika kukupatia mema.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2