Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 23 YA 30

Mwaka wa 50 Paulo alifika Thesalonike, mji mkuu wa Makedonia, kwenye safari yake ya pili ya kueneza Injili, akakaa majuma 3 tu, akafukuzwa na Wayahudi (ukitaka kusoma habari zote, angalia Mdo 17:1-10). Hata hivyo usharika wa kudumu ulianzishwa. Sababu moja ya mafanikio hayo ni maombezi ya Paulo (m.2). Tafakari alama za usharika hai (taz. m.3): 1.Imani itendayo, ikitegemea kazi ya wokovu iliyofanywa na Yesu. 2.Upendo udumuo kusaidia hata panapotokea taabu. 3. Tumaini katika kuja kwa Yesu liletalo faraja na kuwezesha kuangalia mbele kwa saburi.

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz