Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 25 YA 30

Tafakari jinsi nguvu ya Injili ilivyo kuu: Huwapa waipokeao furaha hata wakiwa katika dhiki (1:6), na kuwapa waihubirio ujasiri wa kuendelea kuieneza hata wakipigwa na kuwekwa gerezani (m. 2; ling. Mdo 16:19-25: Wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji. ... Makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza). Ni kwa sababu Injili ni yake Mungu (m.2). Kwa hiyo Paulo alikuwa mtumishi wa wote kwa ajili ya Yesu (ling. 2 Kor 4:5: ... tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu), yaani katika kuwatumikia watu alitafuta kibali cha Yesu wala si kibali chao kwa njia ya kuwapendeza (m.4). Tukifuata kielelezo hicho, pia uinjilisti wetu utakuwa na mafanikio mema kama vile uinjilisti wake (m.1).

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha